Mwili wa Marehemu George Tyson (pichani) utapelekwa nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach (eneo la Makonde) kesho Jumanne Juni 3 kuanzia majira ya saa kumi jioni kwa ajili ya kuaga.
Mwili utakuwepo nyumbani hapo mpaka siku ya Jumatano Juni 4,ambapo mwili utapelekwa kwenye viwanya vya Leaders Club,Kinondoni kwa ajili ya shughuli ya kuaga mwili na ibada fupi.
Baadae mwili utapelekwa kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere tayari kwa kusafirishwa kwenye jijini Nairobi nchini Kenya kwa mazishi.
Tutaendelea kuwaletea taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.
0 Comments