Header Ads Widget

TAZAMA VIDEO:MACHOZI NA VILIO VILIVYOTAWALA UWANJA WA DORTMUND WAKATI LEWANDOSKI ALIVYOAGWA KWENYE KLABU HIYO.

Wakati zikiwa zimebaki siku chache kabla msimu wa Bundesliga haujaisha, weekend hii Borrusia Dortmund ilikuwa ikicheza mechi yake ya mwisho kwenye uwanja wao wa nyumbani Signal Iduna Park dhidi ya Hoffenheim – pamoja na ushindi waliopata siku hiyo, tukio kubwa lilovutia watu ilikuwa sherehe ya kumuaga mshambuliaji wao kipenzi Robert Lewandoski ambaye ataihama timu hiyo mwishoni mwa msimu.

Lewandoski ambaye ni raia wa Poland amemaliza mkataba wake na Dortmund na atajiunga na klabu ya Bayern Munich msimu ujao. Tofauti na wachezaji wengine waliondoka Dortmund ambao walichukiwa na mashabiki – Lewandoski aliagwa vizuri na mashabiki zaidi ya 80,000 waliojazana kwenye uwanja wa Signal Iguna Park, na kumfanya kushindwa kujizuia kutokwa na machozi.

Tazama video namna alivyoagwa Lewandoski

Post a Comment

0 Comments