
Wananchi wa Afrika Kusini leo wanapiga kura kumchagua Rais wa nchi hiyo, ukiwa ni uchaguzi huru wa tano kufanyika baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi miaka 20 iliyopita.
Zaidi ya vituo 22,000 vimeandaliwa nchi nzima kwa ajili ya zoezi hilo la upigaji wa kura, huku mgombea Urais wa Chama cha ANC, Rais Jacob Zuma akiwa na matumaini makubwa ya kushinda uchaguzi huo na kuiongoza Afrika Kusini kwa kipindi kingine cha miaka 5 ijayo.

Hata hivyo Zuma anashutumiwa kwa kuongozeka kwa kiwango cha rushwa pamoja kukosekana kwa ajira nchini humo.
CREDIT:RWEYUNGA BLOG
0 Comments