Header Ads Widget

MWANAMKE KWANINI HUSHIKI MIMBA? HIZI NDIO SABABU ZA KUTOSHIKA MIMBA KWA MAWANAMKE

 THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAKUPA

SEHEMU YA KWANZA
Mtu ambaye ana tatizo la kutoshika mimba kitaalamu tunasema Infertility na kushindwa kupata mimba kwao huitwa Conceive. Kwa kawaida kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, wanandoa asilimia 50 wanapata mimba ikiwa watajamiiana bila kutumia kinga wakifanya tendo hilo ndani ya miezi mitatu na asilimia 75 baada ya miezi sita na asilimia 95 baada ya mwaka mmoja.



Sababu za tatizo la kutopata mimba ni nyingi sana na baadhi yake ni hizi zifuatazo. Matatizo ya mbegu za kiume (Sperm disorders). Asilimia 35 ya wanaume wana tatizo hili na lingine ni kutopevuka kwa mayai kwa wanawake yaani kitaalamu huitwa Ovalatory dysfunction, asilimia 20.

Matatizo mengine ni yale yasiyo ya kawaida ya ute wa shingo ya uzazi ambapo ni asilimia 5 tu, wengine huwa na matatizo ya homoni na wapo ambao hawapati mimba na sababu zao hazijulikani ni asilimia 10, wengine ni kutokana na kuwa na msongo wa mawazo na wasiwasi.

Tatizo lingine la kutoshika mimba husababishwa na hitilafu katika mirija ya uzazi (tubal dysfunction), hawa huwa asilimia 30. Sababu zote hizi nitaeleza moja moja kwa kirefu katika matoleo yetu yajayo lakini wote wenye tatizo hili wanashauriwa kuhudhuria kliniki za akina mama ili waonane na madaktari.

Lakini pia wanashauriwa kufuatilia siku zao za mzunguko wa hedhi na tendo la ndoa mara kwa mara hasa baada ya siku 10 kutoka siku anamaliza hedhi na aanzie siku ya kwanza ya kupata hedhi. Ushauri Wanawake wanashauriwa wawe wanapima joto la mwili asubuhi na jioni kipindi cha kushika mimba na kama litaongezeka kwa nyuzi joto 0.5 wanashauriwa kipindi hicho kufanya tendo la ndoa.
Kwa nchi za Ulaya na Marekani wana kipimo cha kuonesha siku ambayo yai litapevuka, hivyo mtu kuwa na uhakika na siku ya kupata mimba akiamua.

Kipimo hicho kinaitwa Luteinizing hormone prediction test kits. Wanawake wanaotaka kupata mimba wanashauriwa kuepuka ulevi na uvutaji wa sigara wa kupindukia. Lakini hata wale wenye mimba wanashauriwa kuepuka vitu hivyo.

SEHEMU YA PILI
Tatizo la mwanamke kutoshika mimba limegawanyika katika makundi mawili, la kwanza huitwa kitaalamu ‘primary Infertility’.
Kundi hili ni lile ambao mwanamke huwa hajawahi kushika mimba hata siku moja na kundi la pili huitwa ‘Secondary Infertility’, hili ni lile la wanawake ambao wamewahi kushika mimba wakajifungua au mimba zikaharibika.
Zipo sababu nyingi sana zinazofanya mwanamke asiweze kushika mimba kama vile kupata maambukizi katika viungo vya uzazi, hali duni ya lishe na kukumbwa na magonjwa sugu.
Wanawake wengine wanakuwa na matatizo yanayohusu upevushaji wa mayai ambayo kitaalamu huitwa ‘Ovulatory’. Tatizo hili huathiri wanawake kwa kiasi kikubwa ambapo mwanamke anapata siku zake kama kawaida lakini hapevushi mayai.

Hali hiyo husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni mwilini, tatizo linaweza kutokea lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwilini.

Lakini pia tatizo hilo linaweza kujitokeza kutokana na matumizi yanayohusiana na dawa za homoni kutumika kiholela bila kupata ushauri wa daktari na ndiyo maana tunasisitiza kuwa si vema kunywa dawa bila kushauriwa na daktari.

Wanawake wengine wanaweza kushindwa kupata mimba kutokana na matumizi ya baadhi ya vyakula au vipodozi vyenye kemikali.

Ieleweke kwamba wanawake wanaotaka kupata mimba wanakuwa na dalili za upevushaji wa mayai na kubwa ni kupata ute wa uzazi.

Daktari anaweza kuona upevushaji huo kwa kutumia vifaa maalumu ambavyo siku hizi hata mwanamke akiwa nyumbani anaweza kupima mkojo siku unazohisi unaweza kupata mimba.
Matatizo mengine yanayosababisha mwanake asipate mimba ni kuwa na matatizo kwenye mirija kwani inaweza kuziba, kutanuka au kuweka usaha au maji. Maambukizi katika mirija au upasuaji wa mimba nje ya kizazi au kufunga kizazi kunaweza kumfanya mwanamke asipate mimba.

Itaendelea wiki ijayo.

Post a Comment

0 Comments