Header Ads Widget

Waziri Mkuu awataka TANESCO Kufanya Kazi Kwa Bidii

Waziri Mkuu awataka TANESCO Kufanya Kazi Kwa Bidii

Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea maonesho ya nishati

yanayoendelea jijini Dodoma na kuwataka wafanyakazi wa TANESCO kuendelea kuchapa kazi licha ya changamoto mbalimbali ili kupata mafanikio ya utendaji wao.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali zilizoko chini ya Wizara ya Nishati mara baada ya kutembelea maonesho yaNishati yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma ambapo amesemaanaridhishwa na utekelezaji na maendeleo ya miradi ya kimkakati kama bwawa la kufua umemela mwalimu Nyerere unaotekelezwa na TANESCO ambapo mradi umefikia asilimia 86.89.
“Hatuna mashaka na utendaji wenu wa kazi na utaalamu wenu, endeleeni kuchapa kazi,

imarisheni utoaji wa huduma, lugha iwe nzuri kwa wateja tutafika tu” alisema Majaliwa
Akimkaribisha waziri mkuu,Mhe. January Makamba Waziri wa Nishati amesema kwa sasa

serikali kupitia wizara ya nishati inatoa kipaumbele kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikiakwa kushirikiana na ofisi ya makamu wa rais ili kuwahamisha wananchi kutumia nishatimbadala na kuhifadhi mazingira.

Katika hatua nyingine amepongeza watendaji wa TANESCO wanaofanya kazi kwenye maeneombalimbali na kuwataka kuendelea kuwa watoa huduma wazuri kwa wananchi bila kuchoka.

Baadhi ya wabunge waliotembelea kwenye mabanda ya TANESCO kwenye maonesho

yanayoendelea mjini Dodoma ni pamoja na Mhe. Anna Lupembe, Mhe. George simbachawene,Mhe. Prof. Paramagamba kabudi, Mhe. Hussein Bashe, Mhe. Hamis Mwinjuma ambapo kwanyakati tofauti wamesifu hatua iliyofikiwa kwenye utekelezaji wa mradi wa bwawa la kufuaumeme la Mwalimu Nyerere ambapo wamesema pindi utakapokamilika utaleta mapinduzimakubwa kwenye sekta ya umeme nchini.
Waziri Mkuu awataka TANESCO Kufanya Kazi Kwa Bidii
Waziri Mkuu awataka TANESCO Kufanya Kazi Kwa Bidii
Waziri Mkuu awataka TANESCO Kufanya Kazi Kwa Bidii
Waziri Mkuu awataka TANESCO Kufanya Kazi Kwa Bidii
Waziri Mkuu awataka TANESCO Kufanya Kazi Kwa Bidii

Post a Comment

0 Comments