Header Ads Widget

Watu 10 Wafariki Dunia Baada Ya Lori Kuvamia Kituo Cha Waendesha Bodaboda


Picha ikionyesha ajali ya lori lililovamia kituo cha bodaboda
Picha na GPL

Takribani watu 10 wamefariki dunia katika ajali mbaya iliyotokea asubuhi ya leo, April 8, 2023 katika eneo la Migori nchini Kenya, baada la lori kufeli breki nakuvamia kituo cha bodaboda.

Ajali hiyo imetokea katika Barabara ya Migori-Isibiania ambapo kwa mujibu wa mashuhuda, lori hilo lilimshinda dereva na kuwagonga watu waliokuwa kwenye kituo cha bodaboda, wengi wakiwa ni madereva.

“Tuliona lori likija kwa kasi, likaanza kuwagonga watu wa pembeni wakiwemo madereva bodaboda kabla ya kwenda kugonga lori jingine lililokuwa na mchanga,” amekaririwa shuhuda mmoja wa ajali hiyo.

Post a Comment

0 Comments