Timu ya taifa ya Tanzania imeibuka na ushindi wa bao 1-0, ugenini mbele ya Uganda katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon 2023), zitakazofanyika nchini Ivory Coast mwaka huu.
Katika mechi hiyo ya kwanza kwa kocha mpya wa Stars, Adel Amrouche bao pekee na la ushindi kwa Stars lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 68 akimalizia pasi safi ya Dickson Job aliyekuwa aliyecheza eneo la beki wa kulia.
Kwa matokeo hayo Stars imesogea hadi nafasi ya pili kwenye kundi F kwa kufikisha alama 4, Algeria inaoongoza kundi ikiwa na alama 9 , Niger ikiwa nafasi ya tatu na alama 2 na Uganda inaburuza mkia ikiwa na alama 1.
0 Comments