Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa Arusha(APET) Petro Ahham akimkabidhi kikombe cha ushindi wa Bonanza la Amani na Utalii Mkoa wa Arusha,Nahodha wa timu ya Kitambi Noma, James Lugangira.
Wanamichezo wa Kitambi noma wakishabikia ushindi mara baada ya kukabidhiwa kombe katika kiwanja cha General Tyre jijini Arusha.
Na Woinde Shizza,Arusha
Klabu ya Kitambi noma ya jijini Arusha, hivi karibuni ilitwaa ubingwa wa soka katika tamasha la kwanza la amani na utalii ambalo lilifanyika viwanja vya General Tyre jijini Arusha.
Timu hiyo ilitwaa ubingwa baada ya kuzishinda timu za Wazee Klabu na Chuo cha Uandishi wa Habari Arusha (AJTC) kwa kukusanya alama nyingi kutokana na mashindano yaliyoendeshwa kwa mfumo wa Ligi.
Katika tamasha hilo, liliandaliwa na taasisi ya Arusha media jumla ya timu sita zilishiriki katika michezo mbali mbali na sambamba na kutolewa burudani ya ngoma za asili kutoka kikundi cha Cultural Arts Center cha Chuo Kikuu cha Makumira.
Hata hivyo kwa upande wa mpira wa pete, timu ya Wazee Qeen ilifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuichapa katika mchezo wa fainali timu ya AJTC Qeen magoli 34-7.
Katika mchezo wa kukimbiza kuku, timu ya Kitambi noma ilishinda dhidi ya Wazee Klabu na kwa upande wa wasichana AJTC ilishinda dhidi ya Wazee Qeen.
Akikabidhi zawadi za washindi , Mwenyekiti wa Kamati ya Amani mkoa wa Arusha, Petro Ahham alipongeza timu zote zilizoshiriki kutokana kudumisha amani kwa vitendo.
“tamasha hili limekuja wakati muafaka kwani Arusha ni jiji la kitalii ambalo linahitaji amani wakati wote hivyo kufanya michezo kuhimiza Amani na Utalii ni jambo jema sana”alisema
Awali Katibu wa chama cha soka wilaya ya Arusha, Zakhayo Mjema alipongeza taasisi ya Arusha Media kwa kuandaa tamasha hilo la amani na utalii katika jiji la Arusha.
“matamasha kama haya yalipaswa kufanywa na chama cha soka lakini tumekwama hivyo, tunapongeza Arusha Media kwa kusaidia kuendeleza michezo katika jiji la Arusha”alisema.
Tamasha hilo, lilidhaminiwa na Shirika la hifadhi za taifa(TANAPA),kampuni ya vinywaji ya Cocacola, kampuni ya Sunny Safaris, kampuni ya Big Expedition na kampuni ya Marera Lodge &tours.
chanzo:moblog
Bakharesa ajibu tuhuma za Makontena 349 yaliyopita bandarini bila kodi
Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyoripotiwa hivi karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru. Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake ya Bandari ya Dar es salaam hivi karibuni.
Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa zilizoingizwa na kampuni hio ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika katika sakata hilo. Isipokuwa kumetokea upotevu wa makontena yaliyoingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la kuhifadhia makontena(ICD) linalomilikiwa na kampuni hiyo la Azam ICD.
Aidha imebainika kuwa kuna uchunguzi unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Kampuni hiyo (SSB Group of Companies) kuhakikisha wale wote wanaohusika na upotevu huo wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote wa makontena yaliyohusika katika upotevu huo wanawajibishwa.
SSB Group of Companies
Corporate Affairs Department
November 29, 2015

- See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/11/bakharesa-ajibu-tuhuma-za-makontena-349.html#sthash.4BmUkczQ.dpuf
0 Comments