Header Ads Widget

T.I alisema hawezi kumchagua mwanamke kuwa Rais wa Marekani, Kanye West na Jay Z je?





Baada ya kutangaza nia yake ya kugombea Urais wa Marekani kufikia mwaka 2020, Kanye West amekuwa akiweka headlines nyingi zinazohusiana na viongozi wa Siasa.


Mgombea Urais wa Marekani kwa mwaka 2016, Mama Hillary Clinton.


Licha ya rapper T.I kuonyesha wazi kuwa hatotoa kura yake ya Urais kwa Hillary Clinton ambaye ni mgombea Urais mwanamke, Kanye West ameonekana kuwa na nia tofauti kabisa… kwa mujibu wa mtandao wa Buzzfeed, rapper na producer Kanye West ameamua kuwekeza nguvu zake kwa mgombea huyo kwa kuamua kuchangia fedha kuendesha kampeni za mgombea Urais, Hillary Clinton anaegombea Urais kupitia Chama cha Democartic Party, chama alichopo Rais Barrack Obama.


Kanye West & Hillary Clinton.

Japo mtandao wa Buzzfeed, haujaweka wazi ni kiasi gani cha pesa ambacho Kanye West kaamua kutoa kumsupport Mama Hillary, Kanye sio msanii wa kwanza wa HipHop kutoa support hiyo kwa mama huyo… rapper Ja Rule pia hivi karibuni alisikika akisema kuwa support yake kubuwa ameiwekeza kwa mgombea huyo zaidi.


Ja Rule.

Jay Z pia ameonekana akishirikiana na kamati ya kampeni ya Hillary Clinton kwa ukaribu sana, huku kamati hiyo ilitumia zaidi ya dola 15, 000 ambayo ni sawa na milion 34 za Kitanzania kwenye restaurant ya Jay Z ’40/40′ kwa ajili ya catering, chakula na vinywaji mwezi uliopita.


Jay Z & Kanye West.

Wasanii wengine wanaomuunga mkono Mama Hillary Clinton ni Jessica Alba, Matt Damon na Tom Hanks amabo wote pia tunaambiwa wamechangia kwa namna moja ama nyingine kugaramia kampeni za Mama Hillary Clinton.


Jessica Alba.

Post a Comment

0 Comments