Header Ads Widget

UNAAMBIWA KWASASA VIWANDA FEKI VYA KUTENGENEZA MVINYO UNAOHATARISHA AFYA YA BINADAMU VYASHAMIRI WILAYANI ROMBO



Wakazi wa wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wameiomba Serikali kudhibiti ongezeko la viwanda holela vinavyozalisha kienyeji pombe aina ya wine ambayo inatajwa kudhoofisha afya za watumiaji wa pombe hizo.

Utafiti umebaini kuwa baadhi ya watumiaji wa pombe hizo wamekuwa wakitelekeza familia zao na wengine wakitajwa kupoteza maisha kwa kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo.

Umaarufu wa wilaya ya Rombo ni kuwepo kwa ardhi nzuri yenye rutuba inayokubalika kwa kilimo cha ndizi kinachowawezesha wakazi wa eneo hili kujipatia ridhiki, achiliambali zao la Kahawa ambalo ni uti wa mgongo wa wakulima wa mkoa wa Kilimanjaro.

Miaka ya hivi karibu, wilaya ya rombo imegeuka umaarafu wake na kuwa kichaka cha utengenezaji wa pombe aina ya wine ambayo inazalishwa kwa ndizi na kuchanganywa na bidhaa aina ya molassesi inayotajwa kudhoofisha afya za watumiaji.

Uchunguzi umebaini kuwepo kwa zaidi ya aina 40 za waini huku zikionyesha kutodhibitishwa na mamlaka husika,likiwemo shirika la viwango TanzaniaTBS na Mamlaka ya chakula na dawa TFDA.

Hapa ni katika kijiji cha Kahe kata ya Ubetu Kahe wilayani Rombo,ambapo star tv imekutana ana kwa ana na mmoja wa watumiaji wa pombe hii ambayo inadaiwa kuuzwa kwa gharama nafuu kwa shilingi mia 600 tu kwa kila chupa.

Wakazi wa wilaya ya Rombo wanasema ongezeko la viwanda hivyo vimesabisha vijana wengi kuachana na shughuli za uzalishaji mali na kujiingiza katika wimbi la ulevi wa kupindukia.

Ofisi ya ustawi wa jamii katika wilaya ya Rombo ni kielelezo tosha cha kuongezeka kwa idadi ya malalamiko yanayosababishwa na wanaume kutelekeza familia zao kwa sababu yakuendekeza ulevi .

Licha ya uongozi wa wilaya ya Rombo kukiri kuwepo kwa ongezeko la viwanda hivyo, lakini inawataka wamiliki wa viwanda kukamilisha taratibu zinazotakiwa kisheria huku jeshi la polisi likitoa onyo kwa wale wanaojihusisha na ulevi wa kupindukia.

Hata hivyo halmashauri ya wilaya ya Rombo imekuwa ikikusanya ushuru kutoka katika viwanda hivyo ingawa sheria inakataza kutoza ushuru aina yoyote kama bidhaa haijadhibitishwa na mamlaka husika kwa matumizi ya binadamu.

Source: star tv

Post a Comment

0 Comments