Mbele ya mashabiki 36,170 mchezaji Raheem Sterling aliyefunga goli pekee na la ushindi lililoweza kuizamisha timu ya Olympacos ya Ugiriki kwenye mechi za mazoezi zinazoendelea nchini Marekani kwa ajili ya kujiandaa na ligi za nchi zao. Mechi hii iliyochesewa jijini Chacago jimbo la Illinois siku ya Jumapili July 27, 2014 ilikuwa ya kusisimua na iliyojaa upinzani na kushambuliana kwa zamu muda wote. Bao la Liverpool lilianzia kwa Daniel Sturridge aliyempasia mfungaji na kufunga goli la pekee katika mchezo huo ndai ya dakika 5 za mwanzo.
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia bao
Raheem Sterling akishangilia bao lake.
0 Comments