Baada ya kudaiwa kuwa na gundu kufuatia kila mwanaume anayeishi naye kuandamwa na majanga, staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson ameibuka na kukanusha madai hayo akisema hayana ukweli.
Baada ya maneno hayo kutufikia, wanahabari wetu walimsaka Aunt ili kumsikia anazungumziaje taarifa hizo ambapo alitiririka:
“Sina gundu na wanaume jamani, uzuri ni kwamba kila niliyeishi naye kulikuwa na sababu za msingi za kuachana. Siyo Jack Pemba wala Hartmann (Mbilinyi).
“Watu wanazungumza tu bila kujua ukweli, hata kwa Sunday Demonte (mumewe wa sasa), yupo vizuri na hajafungwa kama wanavyosema,” alisema Aunt.
Miongoni mwa wanaume walioogelea katika penzi la Aunt kisha kumwagana kwa sababu tofuati ni pamoja na Mwilu Mwilola ‘Silvanus’, Hartman na Jack Pemba.
>>Ijumaa Wikienda/gpl
0 Comments